Machapisho
UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI JUNI, 2025
PakuaDondoo za tathmini ya Mei, 2025 na mwelekeo wa Juni, 2025:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Mei, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Juni, 2025 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Mei, 2025 vipindi vya mvua viliendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususan yanayopata misimu miwili ya mvua, sambamba na vipindi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo.
- Kwa mwezi Juni 2025, hali ya joto la chini inatarajiwa kupungua katika maeneo mengi ya nchi ikiashiria kuanza kwa msimu wa Kipupwe (Juni-Agosti), 2025. Aidha, vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mwambao wa pwani, ukanda wa Ziwa Victoria, na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki na kusini magharibi.