Machapisho
TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI JULAI NA AGOSTI, 2024
PakuaKatika kipindi cha mwezi Julai hadi Agosti, 2024 vipindi vya ukavu vilivyoambatana na baridi ya wastani hadi baridi kali iliendelea kujitokeza katika maeneo mengi nchini. Hali hii iliweza kusababisha upungufu wa unyevunyevu ardhini, kupungua kwa maji na malisho pamoja na kuwepo kwa hali vumbi. Hata hivyo, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza na kuathiri maeneo ya ukanda wa pwani, kati mwa nchi, nyanda za juu kusini magharibi na maeneo ya maziwa makuu. Ingawa hali ya ukavu iliendelea kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika maeneo ya ukanda pwani, ziwa Victoria na maeneo yenye miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki. Aidha, hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa msimu wa Kipupwe (Juni-Agosti), 2024.