Machapisho

TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI MACHI NA APRILI, 2024

Pakua

Katika kipindi cha miezi ya Machi na Aprili, 2024 vipindi vya mvua viliendelea kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi. Aidha, maeneo mengi yalipata mvua za juu ya wastani hadi wastani ikilinganishwa na wastani wa muda mrefu wa miezi ya Machi na Aprili. Vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo. Hali hii ilisababisha mafuriko, uharibifu wa miundombinu na mali pamoja na vifo. Kwa upande mwingine, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika maeneo machache ya ukanda wa Pwani na nyanda za juu kaskazini mashariki. Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa mvua za Maika, 2024 na Msimu, 2023/2024.