Machapisho

MWELEKEO WA MVUA ZA VULI (OKTOBA-DISEMBA) 2023 KWA MKOA WA GEITA

Pakua

(i)Msimu huu unatarajiwa kutawaliwa na hali ya El Nino ambayo inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mwenendo wa mvua za msimu wa Vuli, 2023.

(ii)Kwa ujumla mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mkoa wa Geita.

(iii)Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya pili ya mwezi Oktoba, 2023.

(iv)Mvua zinatarajiwa kuisha mwezi Januari, 2024.

(v)Upo uwezekano wa kutokea vipindi vya ukavu vya siku kumi (10) au zaidi katika msimu huu wa Vuli.