Taarifa za Hali ya Hewa Kilimo
Jarida la Hali ya Hewa kilimo la Tathmini ya Agosti 1-10, 2025 na Matazamio kwa Kipindi cha Agosti 11-20, 2025
PakuaDONDOO ZA AGOSTI 11 - 20, 2025
- Hali ya ukavu inayotarajiwa itasaidia shughuli za ukaushaji, uvunaji na utunzaji wa mazao katika maeneo mengi nchini pamoja na maandalizi ya mashamba
- Wafugaji wanashauriwa kuhifadhi malisho kwa ajili ya matumizi ya baadae.
- Wakulima wanashauriwa kuanza kuandaa mashamba kwa ajili ya Msimu ujao wa kilimo huku wakiendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa kwa mipango thabiti ya shughuli za kilimo.
Jarida la Hali ya Hewa Kilimo la msimu wa mvua wa Machi hadi Mei 2025
PakuaMUHTASARI
- Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua...
- Mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo ya pwani ya kaskazini (kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mkoa wa Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), kaskazini mwa mkoa wa Kigoma na ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga na magharibi mwa mikoa ya Simiyu na Mara). Aidha, Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na mashariki mwa mikoa ya Mara na Simiyu.
- Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi, 2025 katika maeneo ya kanda ya Ziwa Victoria na pwani ya kaskazini; na katika wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Machi, 2025 katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
- Ongezeko la mvua linatarajiwa mwezi Aprili, 2025.
- Vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani.
- Kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka hivyo kuongeza hatari ya mafuriko hususan katika maeneo yanayoathiriwa na mafuriko.
- Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji.