Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

ISO 9001:2015 Imethibitishwa Kutoa Huduma za Hali ya Hewa kwenye Usafiri wa Anga

MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MENEJIMENTI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

News Image

MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MENEJIMENTI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) na Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO), Dkt. Ladislaus Chang'a  alifungua  mafunzo ya usimamizi wa miradi ya  maendeleo kwa menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yanayoendeshwa na Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA),  ambapo mafunzo hayo yamejikita zaidi  katika usimamizi wa miradi ya uwekezaji wa miundombinu kama “Capital Expenditure (CapEx)”.

 Dkt. Chang'a katika ufunguzi alisema kuwa TMA ikiwa ni Taasisi ya Serikali  iliyopewa majukumu ya kutoa huduma za hali ya hewa, kuratibu na kudhibiti shughuli zote zinazohusiana na masuala ya hali ya hewa nchini. Mamlaka inashiriki pia kutekeleza miradi mbalimbali yenye malengo yanayochangia kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya TMA ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Aidha, alieleza kuwa miongoni mwa miradi ambayo inatekelezwa na TMA ni ikiwemo miradi ya uwekezaji wa miundombinu mbalimbali “Capital Expenditure (CapEx)”, Ujenzi wa Kituo cha Ufuatiliaji wa matukio ya Tsunami (Tsunami Centre), TMA inapata ufadhili wa kujenga vituo vipya vitatu (3) vya kupima hali ya hewa katika anga za juu kupitia mradi wa (SOFF) na nyinginezo nyingi. 

Kwa upande wake Mtiva wa Kitivo cha Mafunzo ya Insia na Sayansi za Jamii, Dkt. Leticia Rwabishungi wa chuo Cha Uhasibu Arusha aliwashukuru sana  TMA kwa kufika  IAA kwa mafunzo  ya usimamizi wa miradi na kusema chuo kina kozi nyingi sio tu Uhasibu bali kozi mbalimbali na kwa ngazi zote hivyo aliwakaribisha kuendelea kupata mafunzo katika chuo cha IAA.