Taarifa za Utabiri
Mvua na ngurumo zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Upepo mkali na mawimbi makubwa vinatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa pwani.
Kwa taarifa zaidi tafadhari pakua......
MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21-30 APRILI, 2021.
Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua na ngurumo.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua katika maeneo machache.
Pwani ya Kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya Kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua na ngurumo katika maeneo machache.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua na ngurumo katika maeneo machache.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vichache vya mvua.
Nyanda za juu Kusini-Magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo machache.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vichache vya mvua katika maeneo machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo machache.
Imetolewa na:
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali pakua...
Dondoo za tathmini ya Machi, 2021 na mwelekeo wa Aprili, 2021:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa hali ya viashiria pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Machi, 2021 na mwelekeo wa viashiria pamoja na mwenendo wa mvua kwa mwezi Aprili, 2021 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Machi, 2021 maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka yalikumbwa na vipindi vya ukavu hususan katika kipindi cha wiki ya kwanza hadi ya tatu, isipokuwa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria ambayo yalipata vipindi vya mvua.
- Maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka yaliendelea kupata mvua za Msimu. Aidha, vipindi vya mvua kubwa pia vimeripotiwa.
- Katika kipindi cha mwezi Aprili, 2021 mvua zinatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo nchini. Hata hivyo, vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo.
- Hali ya joto inatarajiwa kupungua kiasi katika baadhi ya maeneo katika kipindi cha mwezi Aprili, 2021.
- Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua;
Dondoo muhimu za mvua za Masika (Machi – Mei, 2021)
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua katika kipindi cha Machi – Mei, 2021, ushauri kwa wadau wa sekta na mamlaka mbalimbali kama vile Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Utalii na Wanyamapori, Uchukuzi, Mamlaka za miji, Nishati, Maji na Madini, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa. Baadhi ya mambo muhimu katika taarifa hii ni: -
- Mvua za Masika zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara pamoja na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Kigoma (wilaya za Kakonko na Kibondo).
- Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
- Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki ya nne ya mwezi Februari, 2021 hususan katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki na pwani ya kaskazini.
- Vipindi vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza hususan katika mwezi Mei, 2021.
Athari zinazotarajiwa:
- Unyevunyevu wa kutosha kwenye udongo unatarajiwa kuimarisha uzalishaji wa mazao mbalimbali ukiwemo mpunga.
- Uwepo wa malisho na maji ya kutosha kwa ajili ya mifugo na wanyamapori unatarajiwa kupunguza migogoro baina ya wanyama na binadamu.
- Matukio ya magonjwa ya mlipuko na wadudu waharibifu yanaweza kujitokeza kutokana na hali ya unyevunyevu na kutuama kwa maji.
- Ongezeko la maji katika udongo linaweza kusababisha maporomoko ya ardhi na kuathiri shughuli mbalimbali hususan katika maeneo ya wachimbaji madini wadogo.
- Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinaweza kuambatana na mafuriko na kusababisha uharibifu wa miundombinu, shughuli za kijamii kuathirika, upotevu wa maisha na mali.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua
Dar es Salaam |
|||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Tarehe | Hali ya Mchana | Kiwango cha Juu cha Joto | Kiwango cha Chini cha Joto | Mawio ya Jua | Machweo ya Jua | ||
23/04/2021 |
![]() Mvua |
31°C | 24°C | 06:25 | 18:19 | ||
24/04/2021 |
![]() Mvua na Ngurumo |
30°C | 24°C | 06:25 | 18:19 | ||
25/04/2021 |
![]() Mvua na Ngurumo |
28°C | 22°C | 06:25 | 18:19 | ||
26/04/2021 |
![]() Mvua na Ngurumo |
29°C | 24°C | 06:25 | 18:19 |