Taarifa za Utabiri
Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo vinatarajiwa kuendelea katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Songwe, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Kigoma, Tabora, Katavi na Ruvuma
Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua.......
MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21-31 JANUARI, 2021.
Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vichache vya mvua na ngurumo katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo machache.
Pwani ya Kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya Kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua katika maeneo machache.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo.
Nyanda za juu Kusini-Magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua na ngurumo katika maeneo mengi.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua na ngurumo katika maeneo mengi.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali pakua...
Dondoo za tathmini ya Disemba, 2020 na mwelekeo wa Januari, 2021:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa hali ya viashiria pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Disemba, 2020 na mwelekeo wa viashiria pamoja na mwenendo wa mvua kwa mwezi Januari, 2021 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Disemba, 2020 maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka yaliendelea kupata mvua. Aidha, vipindi vya mvua kubwa pia vimeripotiwa.
- Upungufu wa mvua ulijitokeza katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka hususan yale ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki katika kipindi cha mwezi Disemba, 2020.
- Katika kipindi cha mwezi Januari, 2021 mvua za Msimu katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua zinatarajiwa kuendelea. Aidha, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
- Vipindi vya joto vinatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi hususan yale yanayotarajiwa kuwa na upungufu wa mvua.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua;
Dondoo muhimu za mvua za Msimu (Novemba, 2020 – Aprili, 2021)
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka (kanda ya magharibi, kati, nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo yaliyoko kusini mwa mkoa wa Morogoro) katika kipindi cha miezi ya Novemba, 2020 hadi Aprili, 2021. Ushauri na tahadhari umetolewa kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa. Muhtasari wa mwelekeo wa mvua hizo na athari zake ni kama ifuatavyo:
a) Mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka:
- Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Dodoma, Singida, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Njombe, Iringa, Lindi, Mtwara, kusini mwa mkoa wa Morogoro na mashariki mwa mikoa ya Tabora na Katavi. Aidha, maeneo ya mikoa ya Kigoma, Rukwa pamoja na magharibi mwa mikoa ya Tabora na Katavi yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
- Vipindi vya mvua nyingi vinatarajiwa katika miezi ya Januari na Aprili 2021.
- Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba, 2020 kwa maeneo ya mkoa wa Tabora na kutawanyika katika mikoa mingine inayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka katika wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2020.
- Mvua zinatarajiwa kuisha katika maeneo mengi ya magharibi, kati, nyanda za juu kusini magharibi na pwani ya kusini katika wiki ya nne ya mwezi Aprili, 2021, hata hivyo, kwa mkoa wa Ruvuma mvua zinatarajiwa kuisha kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Aprili, 2021.
b) Athari na ushauri
- Hali ya unyevunyevu ardhini inatarajiwa kuwa ya kuridhisha kwa ajili ya kilimo na malisho katika maeneo mengi.
- Matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanaweza kusababisha mafuriko na kupelekea uharibifu wa miundombinu, upotevu wa maisha na mali.
- Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na kutuama kwa maji machafu na uchafuzi wa maji safi.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua
Dar es Salaam |
|||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Tarehe | Hali ya Mchana | Kiwango cha Juu cha Joto | Kiwango cha Chini cha Joto | Mawio ya Jua | Machweo ya Jua | ||
26/01/2021 |
![]() Mvua |
32°C | 25°C | 06:21 | 18:47 | ||
27/01/2021 |
![]() Vipindi vya Jua |
33°C | 25°C | 06:21 | 18:47 | ||
28/01/2021 |
![]() Mvua Nyepesi |
32°C | 25°C | 06:21 | 18:47 | ||
29/01/2021 |
![]() Vipindi vya Jua |
31°C | 25°C | 06:21 | 18:47 | ||
30/01/2021 |
![]() Mvua |
31°C | 24°C | 06:21 | 18:47 |