Machapisho

Utabiri wa hali ya hewa wa siku kumi kuanzia tarehe 21-31 Machi 2020

Pakua

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21 - 31 MACHI, 2020.)

Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vichache vya mvua zinazoambatana na ngurumo katika maeneo machache.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua katika baadhi ya maeneo hususani nusu ya pili ya dekadi.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua zinazoambatana na ngurumo katika baadhi ya maeneo.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vichache vya mvua zinazoambatana na ngurumo katika maeneo machache hususani nusu ya kwanza ya dekadi.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Mvua nyepesi katika maeneo machache.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Mvua zinazoambatana na ngurumo katika maeneo machache.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Mvua zinazoambatana na ngurumo katika baadhi ya maeneo.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Mvua zinazoambatana na ngurumo katika baadhi ya maeneo.

Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua