Machapisho

Mwelekeo wa mvua kwa mwezi Machi, 2020

Pakua

MUHTASARI WA HALI YA HEWA KWA MWEZI FEBRUARI, 2020 NA MWELEKEO KWA MWEZI MACHI, 2020.
Dondoo za tathmini ya Februari, 2020 na mwelekeo wa Machi, 2020:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa hali ya viashiria pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Februari, 2020 na mwelekeo wa viashiria pamoja na mwenendo wa mvua kwa mwezi Machi, 2020 nchini.

a) Mvua za masika katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (ukanda wa ziwa Viktoria, nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na maeneo ya pwani ya kaskazini) zinatarajiwa kuanza katika mwezi Machi.

b) Katika mwezi Februari, maeneo mengi ya nchi yaliendelea kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani. Aidha, vipindi vya mvua kubwa pia viliripotiwa katika kipindi hicho.

c) Mvua za Msimu katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua zinaendelea vizuri katika maeneo mengi na mtawanyiko wake ni wa kuridhisha. Katika kipindi cha mwezi Machi 2020, maeneo mengi yanatarajiwa kuendelea kupata mvua. Aidha, vipindi vya mvua kubwa pia vinatarajiwa kujitokeza.

Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua;