Machapisho

Mwelekeo wa mvua kwa mwezi Februari 2020

Pakua

MUHTASARI WA HALI YA HEWA KWA MWEZI JANUARI, 2020 NA MWELEKEO KWA MWEZI FEBRUARI, 2020.
Dondoo za tathmini ya Januari, 2020 na mwelekeo wa Februari, 2020:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa hali ya viashiria pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Januari, 2020 na mwelekeo wa viashiria pamoja na mwenendo wa mvua kwa mwezi Februari, 2020 nchini.

a) Kwa mwezi Januari, 2020 maeneo mengi ya nchi (yanayopata msimu mmoja pamoja na misimu miwili ya mvua) yaliendelea kupata mvua. Aidha, vipindi vya mvua kubwa pia vimeripotiwa.

b) Mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua hususan katika wiki ya kwanza na kufuatiwa na vipindi vya upungufu wa mvua katika wiki ya pili ya mwezi Februari, 2020. Hata hivyo, vipindi vya mvua vinatarajiwa kuendelea katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Februari, 2020.

c) Mvua za Msimu katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua zinaendelea vizuri katika maeneo mengi na mtawanyiko wake ni wa kuridhisha. Katika kipindi cha mwezi Februari 2020, maeneo mengi yanatarajiwa kuendelea kupata mvua. Hata hivyo, vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza.

d) Vipindi vya joto vinatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi hususan katika nyakati zenye upungufu wa mvua.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali pakua