Machapisho

Utabiri wa hali ya hewa wa siku kumi kuanzia tarehe 11-20 Februari 2020

Pakua

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 11 - 20 FEBRUARI, 2020.)

Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya ngurumo za radi katika maeneo machache.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua katika maeneo machache hususan katika siku tano za mwanzo za kipindi hiki.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua katika baadhi ya maeneo hususan katika siku tano za mwanzo za kipindi hiki.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua zinazoambatana na ngurumo katika maeneo machache hususan katika siku tano za mwisho za kipindi hiki.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Mvua zinazoambatana na ngurumo katika maeneo machache.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Mvua zinazoambatana na ngurumo katika baadhi ya maeneo pamoja na vipindi vifupi vya upepo mkali.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi Mvua zinazoambatana na ngurumo katika baadhi ya maeneo pamoja na vipindi vifupi vya upepo mkali.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Mvua zinazoambatana na ngurumo katika baadhi ya maeneo pamoja na vipindi vifupi vya upepo mkali

Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua.