Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Utafiti na Matumizi

Divisheni ya Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa


Dkt. Ladislaus Chan'ga, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa


Kazi za Divisheni


Divisheni ya Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa inawajibu wa kukusanya na kusambaza ,kuhakikisha ubora,kuchakata na kuhifadhi takwimu mbalimbali za hali ya hewa nchini

Divisheni hii inawajibika kufanya tafiti katika masuala ya hali ya hewa na mambo yanayofanana na hayo kwa minajili ya kulete tija katika masuala ya hali ya hewa na matumizi yake


Aidha, Divisheni hii inahusika kutoa huduma za mabadiliko ya hali ya hewa,kilimo,haidrolojia,mazingira na utafiti,’ Remote Sensing’ na Mfumo wa Taarifa za Kijografia (GIS)’ kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania


Pamoja na yote hayo,divisheni hii inahusika kufuatilia maendeleo ya mazao na mifugo kwa kutumia uangazi wa ardhini na satelaiti na hivyo kutoa ushauri wa kisayansi katika kilimo na taharifa za usalama wa chakula ikishirikiana na Wizara ya kilimo,Mifugo na Uvuvi;Rasilimali maji na utabiri wa mafuriko ikishirikiana na Wizara ya Maji na inashiriki katika jitihada za mpango wa Taifa wa utafiti wa uvunaji maji;Kilimo,Uchafuvi wa hali ya hewa, Masuala ya Mazingira ya nchi ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa na kuongezeka kwa tabia joto ya duniaWeather by Region

© 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.