Habari

Imewekwa: Dec, 11 2020

TMA YATOA MSISITIZO KWA WADAU KUTUMIA VIZURI TAARIFA ZILIZOBORESHWA ZA HALI YA HEWA.

TMA YATOA MSISITIZO KWA WADAU KUTUMIA VIZURI TAARIFA ZILIZOBORESHWA ZA HALI YA HEWA.

Simiyu, Tarehe 08 Disemba 2020:

Mamlaka ya Hali ya Hewa imetoa msisitizo kwa wadau kuhusiana na matumizi ya taarifa za hali ya hewa zilizoboreshwa. TMA ilisisitiza hayo wakati wa warsha ya siku mbili kati ya waandaaji na watumiaji wa taarifa za hali ya hewa iliyofanyika mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Simiyu, kuanzia tarehe 26 Novemba 2020 mpaka tarehe 8 Disemba 2020. Warsha hiyo ilikuwa na lengo la kushirikisha wadau katika uzalishaji wa taarifa za hali ya hewa zilizoboreshwa kwa matumizi katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii, zikiwemo za kilimo, uvuvi, maji, nishati na usimamizi wa majanga.

Warsha hiyo iliandaliwa na TMA ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa WISER (Weather and Climate Information Services for Africa) wenye lengo la kuwaongezea ujuzi wazalishaji na watumiaji wa taarifa za hali ya hewa kwenye sekta mbali mbali ikiwemo kilimo, uvuvi, nishati, maji, na usafiri kwenye maji chini ya udhamini wa Serikali ya Uingereza kwa kushirikiana na taasisi ya hali ya hewa nchini humo.

Aidha, wakati wa warsha hiyo, mambo mbali mbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa takwimu za hali ya hewa, uandaaji wa taarifa za hali ya hewa za muda mfupi, wa kati na mrefu, usambazaji wa taarifa za hali ya hewa, uandaaji wa taarifa za hali ya hewa kwenye maeneo madogo, lugha, tafsiri na mipaka ya matumizi ya taarifa husika, kupokea mirejesho ya wadau juu ya matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwenye maeneo Kwa upande wa washiriki walishukuru Mamlaka kwa juhudi walizozichukua katika kutoa tofauti, pamoja na kuongeza thamani kwa wadau kuweka ushauri na madhara yanayo tarajiwa kwenye taarifa za hali ya hewa zilizo boreshwa.

Pamoja na hayo, washiriki walipata nafasi ya kutoa maoni ya namna bora ya kusambaza taarifa ya hewa ya hewa kwenye maeneo mbalimbali.