Habari

Imewekwa: Sep, 10 2019

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YATOA TAARIFA YA MWELEKEO WA MVUA ZA VULI KWA MWAKA 2019

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YATOA TAARIFA YA  MWELEKEO WA MVUA ZA VULI KWA MWAKA 2019

Mvua za msimu wa Vuli, 2019 Maeneo yanayozunguka ukanda wa Ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani. Maeneo mengine yaliyosalia (Pwani ya Kaskazini pamoja na Nyanda za juu kaskazini. Mashariki), mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani.


Maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi Oktoba, 2019 isipokuwa maeneo machache ya mkoa wa Kagera ambapo vipindi vya mvua za nje ya msimu zilizoanza toka mwezi Agosti 2019, vinatarajiwa kuendelea na hivyo kuungana na kuanza kwa msimu wa mvua za Vuli.