Habari

Imewekwa: Sep, 19 2019

WAZIRI MKUU AZISHUKURU NCHI ZA SADC

WAZIRI MKUU AZISHUKURU NCHI ZA SADC

Tarehe 19/09/2019: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezishukuru nchi wanachama wa SADC kwa kumuunga mkono Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi na kuchaguliwa kuwa makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO). Alizungumza hayo wakati akifungua rasmi mkutano wa mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa, unaofanyika nchini, katika ukumbi mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.

‘Nachukua fursa hii kuzishukuru nchi zote wanachama wa SADC kwa kukubali kumuunga mkono Dkt. Agnes Kijazi na kufanikisha kuchaguliwa kwake kuwa makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani’, alisema Mhe. Majaliwa

Aliongeza kuwa, kumekuwa na changamoto nyingi za mabadiliko ya hali ya hewa na kupelekea kuwa na ongezeko la matukio ya hali mbaya ya hewa kama vile kimbunga Kenneth na kuzitaka nchi hizo kushirikiana na kuboresha miundo mbinu yao, hata hivyo alieleza kuwa katika kukabiliana na hali hiyo Tanzania imeweza kusimika rada mbili za hali ya hewa na rada zingine tatu ziko katika hatua za usimikaji.

Mkutano huo umeanza rasmi tarehe 16 na unaendelea mpaka 20 Septemba 2019 ukijumuisha mawaziri na wataalamu mbalimbali wa sekta husika kutoka nchi za SADC. Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Mazingira Wezeshi kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi na Endelevu, Kukuza Biashara katik Jumuiya na Kuongeza Fursa ya Ajira’