Habari

Imewekwa: Aug, 05 2020

NANENANE 2020: NAIBU WAZIRI WA MAJI AITAKA TMA KUFIKISHA TAARIFA ZAKE MAENEO YOTE NCHINI.

NANENANE 2020: NAIBU WAZIRI WA MAJI AITAKA TMA KUFIKISHA TAARIFA ZAKE MAENEO YOTE NCHINI.

Morogoro; Tarehe 04/08/2020

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuboresha njia za usambazaji wa taarifa za hali ya hewa ili ziweze kuwafikia wananchi maeneo yote nchini kwa vile hivi sasa kuna maeneo taarifa hizo hazifiki. Alizungumza hayo wakati alipotembelea banda la TMA katika maonesho ya NaneNane 2020, Morogoro.

Aidha, Mhe. Aweso aliihasa TMA kuhakikisha kiwango cha usahihi kinaongezeka zaidi kwa vile Serikali imeendelea kuipa uwezo huo TMA kwa kuwapatia vifaa vya uangazi kama vile Rada za hali ya hewa, na kuwataka watumishi wa Mamlaka kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujenga nchi kwa pamoja.

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi katika banda la TMA, msimamizi wa banda na mtaalam wa hali ya hewa wa TMA, Dkt. Alfred Kondowe aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresho mtandao wa vituo vya hali ya hewa ikiwa ni pamoja Rada za hali ya hewa.