Habari

Imewekwa: Sep, 20 2019

BALOZI SEIF AFURAHISHWA NA HATUA YA TMA KUANZA KUTEKELEZA MKATABA WA KUSITISHA MATUMIZI YA ZEBAKI NCHINI.

BALOZI SEIF AFURAHISHWA NA HATUA YA TMA KUANZA KUTEKELEZA MKATABA WA KUSITISHA MATUMIZI YA ZEBAKI NCHINI.

BALOZI SEIF AFURAHISHWA NA HATUA YA TMA KUANZA KUTEKELEZA MKATABA WA KUSITISHA MATUMIZI YA ZEBAKI NCHINI.

Tarehe 20/09/2019: “Nimefurahi kusikia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeanza kutelekeza mkataba wa MINAMATA wa kusitisha matumizi ya zebaki katika vifaa vya hali ya hewa”, alizungumza Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mara baada ya kufunga mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa na kutembelea banda la TMA kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Naye, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe alimueleza Mhe. Balozi Seif kuwa serikali inaangalia namna sahihi ya kuweze kuteketeza vifaa hivyo kiusalama Zaidi, kwa vile zebaki ni moja ya vitu vinavyochangia katika uharibifu wa mazingira.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa alisema kuwa, TMA imeshafanikisha zoezi hilo la kuacha matumizi ya vifaa vyenye zebaki vikiwemo vipima joto (thermometers), vipima mgandamizo wa hewa (barometers) n.k kwa asilimia kubwa kwa kuwezeshwa na serikali upatikanaji wa vifaa ambavyo havitumii zebaki.

Mkutano huo umefungwa rasmi leo tarehe 20 Septemba 2019. Kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa ‘Mazingira Wezeshi kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi na Endelevu, Kukuza Biashara katik Jumuiya na Kuongeza Fursa ya Ajira’

Kwa matukio zaidi kwa picha tembelea: https://meteotz1950.blogspot.com/2019/09/balozi-se...