Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Habari

 • MKUTANO WANAHABARI: MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA TANZANIA KIPINDI CHA MVUA ZA MASIKA MACHI - MEI 2017

  Imewekwa: 28th February, 2017

  Mwelekeo wa msimu wa mvua kipindi cha Machi –Mei, 2017:


  · Katika kipindi cha Machi hadi Mei, 2017 mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, maeneo ya nyanda za juu Kaskazini mashariki (Arusha, Kilimanjaro na Manyara) pamoja na Pwani kaskazini (Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba)msimu wa mvua unatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani zikiambatana na vipindi virefu vya ukavu.

  · Katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria na maeneo machache ya pwani ya Kaskazini mvua zinazoendelea zinatarajiwa kuungana na kuanza kwa msimu wa mvua katika wiki ya kwanza hadi ya pili ya mwezi Machi, 2017 na kusambaa katika maeneo mengine.

  · Kwa upande mwingine, mvua za msimu ambazo zilianza mwezi Novemba 2016 katika maeneo yanayaopata msimu mmoja wa mvua zinatarajiwa kuendelea kunyesha katika kiwango cha wastani hadi juu ya wastani katika mikoa ya (Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi, Mbeya na Iringa).

  · Mvua za juu ya wastani zinatarajiwa kuendelea katika mikoa ya (Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na eno la kusini mwa Morogoro (Mahenge).

  Athari


  · Pamoja na mabadiliko kidogo yanayotarajiwa katika hali ya maji na malisho, vipindi virefu vikavu ndani ya msimu wa mvua vinaweza kuendelea kusababisha upungufu wa maji na malisho kwa mahitaji ya mifugo na wanyama pori hususan katika maeneo yanayotarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani.

  · kutokana na mvua chache zinazotarajiwa katika baadhi ya maeneo, upungufu wa maji unaweza kusababisha milipuko ya magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji salama kwa jamii na matumizi mabaya ya mifumo ya maji taka katika miji.

  · Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinaweza kujitokeza na kusababisha mafuriko na athari mbalimbali zikiwemo athari kwa mazao na shughuli za uvunaji mazao.  Kwa taarifa zaidi ingia humu

  tma swahili

 • Weather by Region

  © 2018 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.