Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Habari

  • WATAALAMU WA HALI YA HEWA KUHAKIKISHA USAHIHI WA UTABIRI WA MVUA ZA MASIKA UNAKUWA WA HALI YA JUU

    Imewekwa: 11th February, 2019

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi amewata wataalam wa hali ya hewa kutumia utalaam wao walionao kuhakikisha maandalizi ya utabiri wa hali ya hewa kwa msimu wa mvua za masika (Machi hadi Mei2019) unaendelea kuwa sahihi zaidi katika kiwango cha juu na wenye ubora utakaosaidia maendeleo ya kiuchumi katika taifa letu. Dkt. Kijazi alizungumza hayo wakati wa kufungua warsha ya wataalamu wa hali ya hewa katika kuandaa utabiri huo.

    Warsha hiyo itafuatiwa na warsha ya wataalamu mabingwa wote wa hali ya hewa pamoja warsha ya wadau wa huduma za hali ya hewa na warsha ya wanahabari kabla ya kutoa rasmi mwelekeo wa msimu wa mvua za MASIKA 2019 tarehe 14 Februari 2019.

  • Weather by Region

    © 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.