Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Habari

 • URITHI WETU

  Imewekwa: 04th October, 2018

  Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii wamejumuika katika kuadhimisha mwezi wa Urithi Festival kwa mkoa wa Dar es Salaam yanayofanyika Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama Tarehe 01 hadi 06 Oktoba 2018

  Katika maonesho hayo TMA ambayo ni taasisi iliyopewa jukumu la kutoa huduma za hali ya hewa nchini imeendelea kutoa elimu namna ya kuulinda na kuutunza urithi wa nchi yetu kwa kutambua faida za matumizi ya taarifa za hali ya hewa.

  Miongoni mwa elimu inayotolewa ni matumizi ya taarifa za hali ya hewa za muda mfupi, kati, mrefu na takwimu za hali ya hewa katika kulinda mali kale mfano majengo ya zamani yaliyo kando ya fukwe za bahari ambapo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa/tabia nchi utafiti unaonesha uwepo wa ongezeko la kina cha bahari hivyo kupelekea uwezekano wa kupotea kwa urithi wa nchi hii. Aidha kuhamahama kwa wanyama kutokana na kutafuta malisho, ikumbukwe kuwa uoto wa asili hutegemea hali ya hewa nzuri kama vile mvua za kutosha

  Vilevile, kwa upande wa kilimo watanzania wana shauriwa kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinafuatwa ili kuweza kuendelea kulima na kuzalisha mazao ya asili kwa jamii. Pamoja na hayo TMA pia hutoa taarifa za hali ya hewa zinazosaidia kuchagua vazi la asili la kuvaa kwa kipindi husika kama vile baridi, joto n.k

  Ngoma na michezo ya asili pia hutegemea hali ya hewa ya eneo husika kama vile upepo mkali, mvua kubwa kwa maeneo ya michezo ya ziwani, viwanjani n.k

  TMA inawakaribisha wananchi wote kufika katika banda lake ili kuweza kujifunza mengi yanayohusu hali ya hewa na maliasili na utalii (urithi wetu)

 • Tovuti Saidizi

  Video Zingine

  © 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.