Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Habari

 • LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU

  Imewekwa: 30th August, 2018

  LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU


  DODOMA.


  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imejumuika na taasisi zingine kuadhimisha wiki ya jeshi la zimamoto na uokoaji kitaifa inayofanyika Jijini Dodoma tarehe 29 Agosti hadi 01 Septemba 2018. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Shiriki kukuza uchumi wa viwanda, funga king’amua moto kwenye kiwanda chako.”


  Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (MB) ambaye alitembelea banda la TMA na kuwapongeza kwa usahihi wa hali ya juu wa utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni na kuwataka waendelee kuboresha ili kufikia viwango vya juu zaidi ya walipo kwa sasa. Mhe. Lugola aliweza kupata maelezo mafupi kutoka kwa meneja wa TMA kanda ya kati Bw. Waziri Omari Waziri ambapo alieleza kuwa taarifa za hali ya hewa ni muhimu kwa shughuli za uokoaji na zimamoto, akitolea mfano taarifa za upepo mkali ambao kwa kiasi kikubwa unaweza kusababisha moto kusambaa kwa kasi (eneo kubwa) au hata kwa watumiaji wa bahari au ziwa kuathirika na mawimbi makubwa vile vile taarifa ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika eneo husika zinasaidia vikosi vya uokoaji kujipanga na vifaa na njia ya uokoaji kutokana na hali ya hewa ya eneo husika. Aliongezea kuwa mchango wa taaarifa za hali ya hewa katika kukuza uchumi wa maendeleo ya viwanda ni pamoja na kutambua hali ya hewa ya eneo husika ili kujua namna ya kuwekeza, mfano mwelekeo wa upepo hii inasaidia kujua jinsi ya kuelekezea uchafu (moshi), kiasi cha uzalishaji kama vile vinywaji baridi kwa kipindi cha baridi au joto, usafirishaji wa mazao ya viwandani hutegemea hali ya hewa ya wakati huo sambamba na miundo mbinu mfano kipindi cha mvua kubwa ambacho husababisha uharibifu wa miundo mbinu hivyo ni vyema mwekezaji akatafuta njia mbadala ya usafirishaji na mengine mengi.

 • Weather by Region

  © 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.