Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services
Mhe. Jenista Mhagama atembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Imewekwa: 22nd October, 2017
Waziri wa Ofisi ya waziri Mkuu:Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (MB) atembelea TMA kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Mfumo wa Tahadhari za Majanga yanayosababishwa na Mabadiliko ya Hali ya Hewa unaofadhiliwa na UNDP. Katika Utekekelezaji wa Mradi huo TMA imejengewa uwezo katika nyanja za wataalamu na miundombinu ya hali ya hewa. Vituo 36 vya hali ya hewa vinavyojiendesha vyenyewe vimefungwa katika maeneo mbalimbali nchini. Uboreshaji huu wa huduma unalenga kuongeza ufanisi katika sekta mbalimbali za kiuchumi kwa ustawi wa jamii.
© 2018 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.