Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Kuhusu Chuo


Kuhusu Chuo

Dira

"Kuwa na wataalamu wa kutosha na wenye ujuzi mahususi katika Masuala ya Hali ya Hewa na Sayansi yake"

Dhima

"Kutengeneza mazingira bora na endelevu ya kujifunzia, ambayo yatawezesha wahitimu kuchangia katika maendeleo ya Maswala ya Hali ya Hewa na Sayansi yake "


Our Motto

“Ufanisi ndio Rafiki yetu”


Historia ya Chuo

Chuo Cha Hali ya Hewa kilianzishwa Mwaka 1978 Dar es salaam baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mwaka 1977.

Chuo kilihamishiwa Mkoani Kigoma Mnamo mwaka 1983 na tangu hapo chuo kimekuwa kikitoa kozi mbalimbali za awali katika taaluma ya hali ya hewa ambazo ni za viwango vya kimataifa kama ambavyoinaelekezwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Chuo cha Hali ya Hewa Kimesajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE)Tanzania kwa usajili wenye namba REG/EOS/025 na kupata leseni ya kufundisha wanafunzi wa ndani na nje ya nchi.

Chuo kinatumia mtaala ambao umethibitishwa na NACTE na ambao unakidhi vigezo na viwango vya shirika la hali ya hewa duniani katika taaluma ya Hali ya Hewa

Chuo cha hali ya hewa kina idadi ya kutosha ya wanataaluma ambao wana viwango vya kimataifa kukidhi mahitaji ya kitaaluma na mbinu za kisayansi ya hali ya hewa

Weather by Region

© 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.