Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services
VIONGOZI TUGHE
Imewekwa: 22nd November, 2018
Halmashauri ya TUGHE ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
na menejiment ya TMA wamejumuika katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa TMA makao makuu,Ubungo Plaza tarehe 22 Novemba 2018. Katika kikao hicho, mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt.Agnes Kijazi
aliwataka viongozi wa TUGHE kuwa vielelezo vya uadilifu kwenye maeneo yao ya
kazi. Aliongezea kuwa ni vyema viongozi wa TUGHE na menejiment
ya TMA kuweka vipaumbele vya ufanisi wa kazi ili kufanikisha maendeleo ya nchi
kupitia huduma za hali ya hewa zinazotolewa na TMA Wakati huo huo alisisitiza haki iende sambamba na wajibu kwa
kuzingatia utendaji kazi wa pamoja (team work) Kwa upande wa TUGHE katibu wake,bw.Benjamin Bikulamchi
alishukuru Menejiment ya TMA kwa ushirikiano uliopo baina yao pamoja na kutoa
pongezi kwa kazi nzuri inayofanyika katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi Kikao hicho cha siku moja kilijadili masuala mbalimbali kwa
manufaa ya Mamlaka kwa ujumla
© 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.