Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Utabiri


Wataalamu wa Hali ya Hewa wakiandaa Utabiri wa Hali ya Hewa katika kituo kikuu cha utabiri


Kuhusu Utabiri wa Hali ya Hewa

Taarifa kuhusu hali ya hewa inayotarajiwa katika siku mbili tatu zijazo hujulikana kama “utabiri wa hali ya hewa wa muda mfupi” wakati taarifa kuhusu takribani siku kumi huitwa “utabiri wa hali ya hewa wa muda wa kati”; taarifa kuhusu hali ya hewa kiujumla inayotarajiwa katika kipindi kirefu zaidi hujulikana kama “matazamio”.


Zaidi ya utabiri wa hali ya hewa wa muda mfupi, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania hutoa utabiri wa hali ya hewa wa siku kumi, matazamio ya mwezi mmoja na yale ya miezi mitatu (yaani msimu) ijayo. Taarifa hizi za hali ya hewa ni muhimu kwa ajili ya mipango ya muda wa kati na ile ya muda mrefu ya shughuli za kiuchumi na kijamii.


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kupitia kituo chake kikuu cha utabiri inatoa utabiri wa siku 10, Matazamio ya Mwezi na Matazamio ya Msimu

Weather by Region

© 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.