Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Kuhusu TMS

THE TANZANIAN METEOROLOGICAL SOCIETY

(TMS) ni Jumuiya ya wataalam wa sayansi ya hali ya hewa na maji iliyoanzishwa ikiwa na jukumu la kujenga, kuendeleza, kukuza na kusambaza ujuzi wa kisayansi na taaluma ya hali ya hewa, maji na maeneo mengine yanayohusiana na sayansi hiyo pamoja na hatua zote za matumizi yake nchini Tanzania.

Malengo ya Tanzanian Meteorological Society ni:

(1)Kujenga, kuendeleza na kusambaza ujuzi wa kisayansi na taaluma ya Hali ya hewa, maji na maeneo mengine yanayohusiana na sayansi hiyo kwa matumizi katika nyanja nchini Tanzania.

(2) Kukuza matumizi ya sayansi ya halia ya hewa na maji pamoja na maeneo mengine yanayohusiana na sayasi hiyo katika kuchochea maendeleo ya haraka katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.

(3)Kuongeza mwamko wa elimu na mafunzo katika Sayansi ya hali ya hewa na maji na maeneo mengine yanayohusiana na sayansi hiyo nchini Tanzania.

(4)Kutoa ushauri wa kitaaluma kwa watu binafsi, mashirika na taasisi juu ya hali ya hewa na masuala yanayohusiana na hali ya hewa.

(5) Kukuza ushirikiano na jumuiya nyingine za kitaalam katika sayansi ya hali ya hewa na maji, na maeneo mengine yanayohusiana na sayansi hiyo.

Jumuiya ya Wataalam wa Sayansi ya Hali ya Hewa (TMS) imekekuwepo nchini tangu mwaka 1987, na kwa sasa inaendelea kuimarisha mpango na utekelezaji wa shughuli zake. Mpango huu ni pamoja na kuhamasisha na kusajili wanachama zaidi, kuanzishwa kwa tuzo ya TMS Academic Excellence, kukuza Utafiti na Uelewa wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa kwa wanafunzi wa Sekondari nchini kote, na kuimarisha ushiriki wa Wanachama wa TMS katika kufundisha Sayansi ya Hali ya Hewa katika taasisi mbalimbali nchini .

Weather by Region

© 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.