Habari

Imewekwa: Nov, 05 2019

TMA YATOA ELIMU YA NAMNA TAARIFA ZA HALI YA HEWA ZINAVYOWEZA KUSAIDIA KUKUZA SEKTA YA UWEKEZAJI NCHINI.

TMA YATOA ELIMU YA NAMNA TAARIFA ZA HALI YA HEWA ZINAVYOWEZA KUSAIDIA KUKUZA SEKTA YA UWEKEZAJI NCHINI.

Mtwara, Tarehe 31 Oktoba - 02 Novemba, 2019; TMA ilishiriki katika kongamano la uwekezaji na maonesho ya biashara yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu, Mtwara . Ushiriki wa TMA katika maonesho hayo ulikuwa ni kutoa elimu kwa wadau mbalimbali walioweza kutembelea katika banda lake lililokuwa katika maonesho hayo, aidha TMA ilitumia njia ya vyombo vya habari kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Lengo kuu la Mamlaka lilikuwa ni kuwaelimisha wananchi na wawekezaji jinsi ya kuboresha uwekezaji nchini kwa Kufanya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa.

Kwa upande mwingine, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika hotuba yake alisisitiza taasisi za serikali kushirikiana kwa karibu na kituo cha uwekezaji Tanzania kuhakikisha malengo ya kupata wawekezaji wengi hapa nchini yanafanikiwa

kwa matukio zaidi kwa picha tembelea: https://meteotz1950.blogspot.com/2019/11/tma-yatoa-elimu-ya-namna-taarifa-za.html