Habari

Imewekwa: Sep, 17 2019

MKUTANO WA MAWAZIRI WA TEHAMA, HABARI, UCHUKUZI NA HALI YA HEWA SADC

MKUTANO WA MAWAZIRI WA TEHAMA, HABARI, UCHUKUZI NA HALI YA HEWA SADC

Tarehe 16/09/2019:‘Mkutano huu ni fursa kwa huduma za hali ya hewa nchini kwa vile utajadili masuala mbalimbali yenye lengo la uboreshaji, hivyo Tanzania itatumia fursa hiyo kuongeza ufanisi’, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Kijazi, alizungumza hayo wakati wa mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa, ulioanza nchini, katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Aliongezea kwa kusema kuwa Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekuwa ikifanya vizuri katika ukanda wa nchi za SADC ikiwa ni pamoja na kusaidia nchi zingine wanachama wa SADC katika kuboresha huduma za hali ya hewa kama vile kuanzisha mifumo ya kiutendaji bado TMA inajikita katika kuongeza fursa za ajira na kuweka mazingira wezeshi katika ukuaji wa uchumi wa nchi na jumuiya kupitia huduma za hali ya hewa

Aidha katika kuhakikisha TMA inashiriki kikamilifu mkutano huo, TMA imeweka banda maalumu kwaajili ya kuelimisha huduma inazozitoa na mifumo iliyopo sambamba na utabiri mahsusi kwa washiriki wa mkutano

Mkutano huo umeanza rasmi leo tarehe 16 mpaka 20 Septemba 2019 ukijumuisha mawaziri na wataalamu mbalimbali wa sekta husika kutoka nchi za SADC. Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Mazingira Wezeshi kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi na Endelevu, Kukuza Biashara katik Jumuiya na Kuongeza Fursa ya Ajira’

Kwa matukio zaidi ya picha ingia: https://meteotz1950.blogspot.com/2019/09/dkt-kijazi-mkutano-wa-mawaziri-wa-sadc.html