Habari

Imewekwa: Oct, 16 2019

MHESHIMIWA ISSA HAJI USSI GAVU AITAKA TMA KUONGEZA MBINU ZA KUFIKISHA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA WAKULIMA KWA WAKATI.

MHESHIMIWA ISSA HAJI USSI GAVU AITAKA TMA KUONGEZA MBINU ZA KUFIKISHA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA WAKULIMA KWA WAKATI.

Tarehe 14/10/2019 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Issa Haji Ussi Gavu aliwataka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuongeza mbinu za kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa wakulima kwa wakati, alizungumza hayo alipotembelea banda la TMA lililopo kwenye maonesho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya Chamanangwe kisiwani Pemba Tarehe 10 hadi 16 Oktoba 2019. “Ninawataka muongeze mbinu za kuhakikisha taarifa zenu zinawafikia wakulima kwa wakati” alisisitiza Mhe. Issa

Aidha, Mheshimiwa Issa ameipongeza TMA kwa juhudi kubwa inayoifanya na kufanikiwa kuongeza usahihi wa taarifa za hali ya hewa hapa nchini. Maonesho hayo yamefungwa rasmi Tarehe 15 Oktoba 2019 na makamu wa pili wa Rais, baraza la mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.

Kwa matukio zaidi katika picha tembelea: https://meteotz1950.blogspot.com/2019/10/mheshimiwa-issa-haji-ussi-gavu-aitaka.html