Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Habari

 • MSIMU WA MVUA NDJFMA

  Imewekwa: 18th October, 2018

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu kuanzia mwezi Novemba, 2018 hadi Aprili, 2019 katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za TMA. Mkutano huo uliudhuriwa na wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa TMA wakiongozwa na mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi

  Taarifa hiyo inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua (kanda ya magharibi, kati, nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo yaliyoko kusini mwa mkoa wa Morogoro) katika kipindi cha miezi ya Novemba, 2018 hadi Aprili, 2019. Aidha, taarifa imeendelea kwa kutoa mrejeo wa mvua za Vuli katika maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria, pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini-mashariki.

  Vile vile, ushauri na tahadhari umetolewa kwa wadau wa sekta mbali mbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na wanyamapori, maliasili na utalii, uchukuzi na mawasiliano, nishati na maji, mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa. Kusoma zaidi ingia humu ndj &fma 2018 19 draft swa 12 10 2018

 • Weather by Region

  © 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.