Wasifu

Dkt. Agnes Kijazi

Mkurugenzi Mkuu

Dkt. Agnes Kijazi

Dkt. Agnes Lawrence Kijazi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na ni mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani ( WMO).

Dkt. Agnes L Kijazi ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, hivyo Dkt. Kijazi ni miongoni mwa viongozi wa juu kabisa wanne katika uongozi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Dkt Kijazi ana shahada ya uzamivu na ni mtaalamu mwandamizi na mbobezi katika sayansi ya hali ya hewa, Dkt kijazi amebobea katika operesheni mbalimbali za hali ya hewa na amefanya tafiti nyingi za kisayansi hususani katika taaluma ya hali ya Hewa na ametoa machapisho kadha wa kadha ambayo yanatambulika kimataifa.

Dkt. Kijazi anajulikana sana kitaifa , kikanda na kimataifa katika uongozi, aidha Dkt. Kijazi ni mlezi wa kisayansi na kiongozi katika kuhakikisha haki na usawa wa kijinsia unapatikana na kuzingatiwa katika taaluma ya hali ya hewa duniani