Wasifu

Dr Ladislaus Chang'a (PhD in Meteorology )
Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa
Dr Ladislaus Chang'a (PhD in Meteorology )

Dkt. Ladislaus Chang’a ni Afisa Mwandamizi wa hali ya hewa na ni Mkurugenzi wa Divisheni ya Utafiti na matumizi ya hali ya hewa katika Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Amefanya kazi katika taaluma hii ya hali ya hewa tangu mwaka 1995. Dkt. Chang’a ni Mratibu wa Tanzania katika Shirikisho la Kimataifa la Mabadiliko ya hali ya hewa na ni Mwenyekiti mwenza wa Timu ya Kitaalamu ya ufuatilikaji wa hali ya hewa na ni Mjumbe wa Timu ya kuratibu utekelezaji mfumo wa mawasiliakno ya taarifa za hali ya hewa ‘ICT-CSIS’ inayosimamiwa na Kamisheni ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani ya Klimatolojia.

Dkt. Chang’a pia ni Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Mafunzo ya mabadiliko ya hali ya hewa cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni mwalimu wa muda wa ziada katika Chuo hicho. Anahusika pia kuratibu shughuli za Programu ya Kidunia ya hujduma za hali ya hewa ‘GFCS’ katika Tanzania. Alishiriki katika shughuli za utafiti na miradi inayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa, na umuhimu w elimu ya jadi katika utabiri wa hali ya hewa na namna ya kukabiliana. Dkt. Chang’a alishiriki katika Kuandaa mawasiliano ya mwanzo ya Kitaifa katika Fremweki ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ‘UNFCCC’ na kuandaa mikakati ya kitaifa yay a mabadiliko ya hali ya hewa , mikakati ya kitaifa ya mawasiliano, na kufanya mirejeo ya taarifa za Paneli ya Kimataifa ya Mabadiliko ya hali ya hewa ‘IPCC reports’ review of the IPCC reports (AR4 and AR5, SR1.5).